F Zaidi ya wadau 500 kushiriki kongamano la uchumi jumuishi Mbeya | Muungwana BLOG

Zaidi ya wadau 500 kushiriki kongamano la uchumi jumuishi Mbeya


Zaidi ya wadau 500 wanatarajiwa kushiriki katika kongamano la Kigoda cha Uprofesa cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere litakalofanyika tarehe 18 Septemba 2025 kuanzia saa tano asubuhi katika ukumbi wa Nkurumah Lecture Theater, Chuo Kikuu cha Mzumbe – Ndaki ya Mbeya.

Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kigoda cha Uprofesa cha Mwalimu Julius Nyerere katika Taaluma za Umajumui wa Afrika, kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia katika Sekta ya Umma na Binafsi (PPP Center).

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Profesa Alexander Makulilo, amesema uhitaji wa kongamano hilo umetokana na kuzinduliwa kwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Julai 17, 2025 jijini Dodoma.

Miongoni mwa wazungumzaji wakuu watakaoshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa; Mkurugenzi Mtendaji wa PPP Centre, Ndugu David Kafulila; Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Dkt. Gladness Salema; Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, Dkt. Mwajuma Hamza; pamoja na wataalamu kutoka vyuo vikuu vya ndani.

Mjadala utaongozwa na  Mgoda, huku Mwenyekiti wa Kongamano akiwa Profesa Makuliro.

 



 

Post a Comment

0 Comments