F Mwenyekiti UWT Wilaya ya Njombe awataka wanawake kujitokeza kupiga kura "Msiogope Vitisho" | Muungwana BLOG

Mwenyekiti UWT Wilaya ya Njombe awataka wanawake kujitokeza kupiga kura "Msiogope Vitisho"



Mwenye wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Njombe Betrece Malekela ametoa wito kwa wanawake wilayani humo kuto kuogopa vitisho huku wakitakiwa kujitokeza kupiga kura Oktoba 29.

Ametoa wito huo wakati akiwa na Kamati ya utekelezaji Kata ya Kitisi halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe 

Katika ziara hiyo ameweza kuwakumbusha wanawake kujitokeza kwa wingi kupiga kura za Rais, Mbunge na Madiwani.

Hata hivyo amewaeleza wanawake kuwa wasiogope vitisho vya watu wanaotishia kuwa uchaguzi hautakuwepo kwani uchaguzi utakuwepo na kutakuwa na ulinzi wa kutosha. 

Aidha amewataka kuwa makini na na kuvitunza vitambulisho vya kupigia kura kwa kuwa ndiyo itakayowapa nafasi ya kuchagua kiongozi wanaomtaka.


Post a Comment

0 Comments