Mshiriki wa Bongo Star Search (BSS) 2025 Prisca Gretu maarufu kama Prisca BSS kutoka mkoani Manyara, ametoa misaada mbalimbali kwa wazee na wasiojiweza katika Kituo cha Wazee Sarame, Magugu wilayani Babati mkoani Manyara, ikiwa ni sehemu ya shukrani zake kwa jamii.
Prisca amesema msaada huo ni sadaka yake kwa wazee na pia ni njia ya kushukuru jamii ya mkoa wa Manyara pamoja na wadhamini kwa sapoti kubwa waliyoonesha wakati wa mashindano ya BSS Season 15, 2025, ambapo aliingia hatua ya 10 bora kati ya washiriki kutoka nchi za Afrika Mashariki.
“Niliona ni muhimu kushukuru kwa vitendo kwa kuwa bila kura na sapoti yenu nisingefika mbali. Hii ni mwanzo tu, nitaendelea kugusa makundi yenye uhitaji katika jamii,” alisema Prisca.
Prisca aliambatana na wadau mbalimbali wakiwemo wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) pamoja na timu ya Eliana Day Care katika kupeleka misaada hiyo.
Aidha, ameahidi kuendeleza utaratibu huo kwa kugusa makundi yenye uhitaji tofauti ikiwemo watoto, vijana na watu wenye ulemavu.
0 Comments