NA REBECA DUWE,TANGA
Mkuuu wa Tanga Balozi Dkt Batilda Burian ametoa Onyo kali kwa yeyote atakayejaribu kuvurugika kwa amani mtu yeyote atakayetia doa katika kipindi cha uchaguzi kwamba serikali haitaweza kumvulia mtu ambaye ataenda kufanya jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya nchi.
Balo
zi Batilda aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini na viongozi wa Siasa hivi leo ofisni kwake ikiwa ni ujumbe wa kuhimiza kudumisha Amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais ,Wabunge na madiwani ambao utafanyika tarehe 29 October mwaka huu.
Alisema kuwa wananchi wote wanapaswa kujua kuwa serikali imejipanga kuwa Amani inaendelea kuwepo kwa kipindi cha uchaguzi hivyo wanatakiwa kuondoa wasiwasi ambao unasababishwa maneno ya mitandaoni badala yake wanapaswa kujitokeza kupiga kura kwani vyombo vya ulinzi tayari vimejipanga vizuri.
Aidha alisema kuwa wananchi watapiga kura kwa Amani na utulivu bila kubughudiwa hivyo kila mmoja ajue kutakuwa na usalama wa kutosha hivyo wanapaswa kuendelea kudumisha amani na mshikano ambayo ndio sifa ya nchi yetu.
Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la polisi Kamishna msaidizi wa polisi ACP Almachius Mchunguzi Polisi mkoa wa Tanga Almachius wamejipanga vizuri kuhakikisha usalama unakuwepo siku ya tarehe 29 October mwaka huu ambapo ndio siku ya uchaguzi mkuu hivyo wananchi waondoe wasiwasi.
Aliongeza kusema wananchi kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura kwa kutakuwa amani ya kutosha wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi .
samabamba na hayo alitoa wito kwa wananchi wote kujiepusha na vikundi ambavyo vinajitoa mtandaoni kuhatibu amani na endapo atagundulika mtu yeyote wa kufanya hivyo hatasahau atakachofanyiwa na wala wasijaribu.
kwa upande wake Mgombea ubunge kupitia Chama cha wananch CUF Musa Mbarouk akizungumza kwa niaba ya viongozi wa siasa alisema kuwa wananaishukuru serikali kwa kuendelea kuilinda amani kwa kampeni zao zote wamefanya kwa amani na utulivu.
0 Comments