F Ummy Nderiananga aomba kura za CCM Hanang' | Muungwana BLOG

Ummy Nderiananga aomba kura za CCM Hanang'



Na John Walter Hanang'.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi UWT Taifa Kanda ya Kaskazini na Mbunge Viti maalumu watu wenye Ulemavu Ndg. Ummy Nderiananga, amewataka wananchi wa Jimbo la Hanang kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Mgombea Urais wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Ubunge Asia Halamga  na madiwani wote wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jimboni humo, Ummy amesema Dkt. Samia amefanya kazi kubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, barabara na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, hivyo anastahili kupewa kura za kishindo ili aendelee na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye dira na moyo wa upendo, ameleta mageuzi makubwa katika kila sekta. Ni jukumu letu kumpa kura nyingi ili aendelee kuijenga Tanzania yetu,” alisema Ummy.

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Hanang, amewahakikishia wananchi ushindi mkubwa wa CCM kutokana na imani kubwa waliyonayo kwa chama hicho na kazi zilizofanywa na serikali.

“Tunakwenda kushinda kwa kishindo. Wananchi wameona kazi, wameguswa na maendeleo, na wanajua CCM ndiyo chaguo sahihi,” alisema Halamga.

Shughuli hiyo ilipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa vikundi vya ngoma za asili, muziki na vikundi vya vijana, vilivyowasha moto wa kampeni kwa hamasa kubwa.

Post a Comment

0 Comments