Mwenyekiti UWT Wilaya ya Njombe Betrece Malekela ameshiriki mkutano wa kampeni za Mgombea wa Ubunge Jimbo la Lupembe katika kijiji cha Ihang'ana wilayani humo.
Akiwa katika kampeni hizo amesema kuwa wananchi kujitokeza kupiga kura kwa Rais, Mbunge na Diwani kwa wingi ndiyo chanzo cha maendeleo kwenye Jimbo hilo.
Ametaka wananchi kujitokeza kupiga kura ambapo amesema pia kura husaidia kutengeneza historia kwa taifa na mtu binafsi kwamba mimi mwaka 2025 nilipiga kura na ninajivunia kuwa mzalendo kwani nilitimiza haki yangu ya msingi kikatiba hivyo amewaomba wapige kura ili watengeneze Historia.
0 Comments