Mchango huo unaonesha namna kampuni hiyo inavyoendelea kutumia programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kuwekeza katika maeneo yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya wananchi. Safari hii, msisitizo umewekwa katika afya na ustawi wa mama na mtoto, kundi linalohitaji mahitaji maalumu na uangalizi wa karibu katika kipindi cha baada ya kujifungua.
Kupitia makabidhiano hayo, hospitali imepokea vifurushi vyenye pampasi, nguo za watoto, nepi (diapers), sabuni, pedi maalumu za uzazi (maternity pads), vifaa vya usafi pamoja na wipes. Vifaa hivyo vinalenga kurahisisha upatikanaji wa mahitaji ya msingi kwa akina mama na watoto, huku vikichangia katika kuimarisha usafi na utunzaji wa watoto wachanga.
Akizungumzia umuhimu wa mpango huo, Nancy Ingram kutoka Meridianbet amesema kuwa kusaidia jamii zenye uhitaji ni miongoni mwa misingi muhimu ya kampuni hiyo. Ameeleza kuwa kampuni inaamini kuwa biashara inaweza kuwa na mchango mkubwa zaidi inapounganisha shughuli zake na juhudi za kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Makabidhiano hayo yamefanyika kupitia ushirikiano kati ya Meridianbet na uongozi wa Hospitali ya Sinza Palestina, chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Ushirikiano huo unalenga kuimarisha mazingira ya utoaji huduma kwa akina mama na watoto, sambamba na kuonesha nafasi ya sekta binafsi katika kuunga mkono juhudi za taasisi za umma.
Katika kipindi cha baada ya kujifungua, mahitaji kama nepi, sabuni, wipes na pedi za uzazi ni sehemu muhimu ya maandalizi ya kumtunza mama na mtoto. Hivyo, msaada huo unakuja kuongeza nguvu katika upatikanaji wa vifaa vinavyoweza kurahisisha huduma na kupunguza baadhi ya gharama za mahitaji ya msingi kwa wanufaika.
Kwa Meridianbet, kugusa maisha ya jamii ni sehemu ya dhamira inayoendelea kupewa nafasi kupitia shughuli zake za CSR. Kampuni hiyo inaendelea kusisitiza umuhimu wa uwajibikaji unaozidi mipaka ya biashara, kwa kuunga mkono juhudi zinazolenga kuboresha afya, ustawi na maisha ya wananchi, huku ikijenga ushirikiano wenye manufaa na taasisi mbalimbali nchini.


