Maneno mapya unayopaswa kuyatumia wakati wa kutongoza


Ili uweze kumpata kirahisi mwanamke unayemtaka unatakiwa kujifunza mbinu mpya za kutongoza. Wengi wanashindwa kuwapata watoto wanaowapenda kwa sababu ya kutumia maneno ya kawaida au ambayo yamepitwa na wakati.

Hivyo ili uweze kumpata mwanamke unayempenda kwa dhati basi unatakiwa kujifunza kutumia maneno yafuatayo;

1. Nipe makinikia ya moyo wako.

2. Naahidi kulipa mirahaba yako na kodi zote za mapenzi.

3. Sitakudanganya kiwango cha madini kilichoko kwenye mchanga wa madini ya mapenzi kama acacia.

4. Please usizuie contena la mchanga wa madini ya penzi langu kwenye bandari ya moyo wako.

5. Usiniundie kamati za marafiki zako kufanya uchunguzi wa makanikia ya upendo wangu.

6. Usinitangaze kuwa naiba utajiri wa mgodi wa moyo wako hadharini mbele ya vyombo vya habari.

7. Nitakuomba ukae kwenye meza ya mazungumzo ili uniruhusu kuchimba sukari ya moyo wako.

8. Usiwahusishe viongozi wastaafu ma X wako katika katika ombi langu sababu wengine watakuwa walikusainisha mikataba mibovu ikakuumiza na wengine wamepumzika baada ya kazi kubwa ya kulijenga taifa la moyo wako.

Endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati


Post a Comment

0 Comments