Inasikitisha sana
kuona chama kilichokuwa na sifa hapa nchini kupinga vita ufisadi na rushwa,
ndio kinakuwa chama kikuu cha kupokea mafisadi ya kila namna. Inasikitisha sana hasa ikizingatiwa
kuwa Mafisadi haya yanajiunga na chama hiki baada ya kukatwa kutoka CCM.
Mtu kama Lowassa, ameondoka
CCM sababu ya kukatwa na sio ameondoka kwa kupiga vita rushwa na ufisadi.
Lowassa hana mapenzi ya dhati na CHADEMA. Lowassa ni kama
mtu anayeshika mwamvuli wakati mvua inanyesha, ili asilowane maji. Lowassa
amenyeshewa mvua CCM kakimbilia mwamvuli ambao ni CHADEMA.
Hakika kwa hili CHADEMA wamepoteza mwelekeo kabisa, ni kama mbwa anapoamua kula matapishi yake mwenyewe! Kwa
hili wamewakatisha tamaa Watanzania waliokuwa wanawaamini kuwa wapo kwa ajili
ya kupambana na rushwa na ufisadi na sio kuwakumbatia mafisadi. CHADEMA
walipaswa kuwa makini sana na maamuzi yao .
Mimi binafsi simlaumu Lowassa kwenda CHADEMA bali nawalaumu sana CHADEMA kukosa
msimamo dhabiti. Lowassa ameingia CHADEMA ili kujaribu kutimiza ndoto zake
binafsi za kuingia Ikulu na sio eti ana mapenzi na CHADEMA. Lowassa ana uchu wa
madaraka, na sababu ameyakosa CCM sasa anajaribu kama
atayapata CHADEMA. Mtu kama huyu ni hatari sana ,
na viongozi wa CHADEMA walipaswa kulibaini hili mapema sana .
Binafsi naamini kabisa ndani ya CHADEMA wapo watu wenye upeo
wa kufikiri na kuchambua mambo, ambao tayari wameshahoji hili swala na
watachukua maamuzi sahihi kabisa, hata kama
hawataondoka CHADEMA lakini kura zao hawatampa huyu Fisadi Lowassa siku
ikifika.
Mtu ambaye hawezi kuzisimamia kauli zake mwenyewe, kamwe
hataweza kusimamia matakwa ya watu wengine pia. Lowassa ameonyesha dhahiri
kabisa kuwa ni mtu mwenye kigeu geu. Mtu kama huyu kuwa Rais ni hatari sana . Kwa kauli yake
mwenyewe alisema kamwe hataondoka CCM, tena akasisitiza kuwa mtu asiyemtaka
ndio aondoke CCM. Lakini cha ajabu yeye ndio amekuwa wa kwanza kuondoka.
Leo hii anasema anataka kuwa rais ili awakomboe Watanzania
kutoka kwenye lindi la umaskini. Hivi kigeu geu kama huyu ambaye bado hajaupata
huo urais ameshaonyesha kutoaminika na kauli zake mwenyewe, je, akiwa Rais
tutaamini vipi kuwa hatageuka na kufanya mambo anayoyataka yeye kwa faida yake
na marafiki zake ambao pasipo shaka wote tunajua kuwa ni mafisadi kama yeye???? Hivi CHADEMA tutawaamini vipi tena kama wameshindwa kusimamia kauli zao sasa hivi, je
itakuwa vipi hawa CHADEMA watakaposhika madaraka ya nchi na kuwa chama tawala??
Nimesikitika sana
kuona chama nilichoamini kuwa ni chama bora cha upinzani sasa kimegeuka na kuwa
pango la wanyang'anyi. Hivi inawezekana kweli mbwa mwitu akaingia kwenye kundi
la kondoo na kuwa mchungaji wa kondoo na kondoo wakabaki salama??? Tuache
ushabiki, tukubali ukweli, kwa hili CHADEMA wamechemka mbaya! CHADEMA
wamewafanya Watanzania kama chapati. Unaigeuza
upande huu kisha unaigeuza upande wa pili au wamewafanya Watanzania kama samaki, unamla upande huu kisha unageuza upande wa
pili pia unakula!
Ukweli ni kwamba kama
itatokea Lowassa akashinda urais(ingawa naamini hawezi kushinda urais), ushindi
utakuwa ni wa Lowassa na friends of Lowassa na hautakuwa ushindi wa CHADEMA.
Ushindi utakuwa ni wa Lowassa na familia yake na wale wote atakaotoka nao CCM.
Lowassa atakuwa na kiburi mbaya sana
sababu itajulikana wazi kabisa bila ya yeye CHADEMA si lolote, si chochote.
Ingekuwa bora mara elfu kama CHADEMA
wangemsimamisha mtu mwingine mbali na Lowassa na kushinda uchaguzi hapa
tungesema CHADEMA wameshinda urais.
Najua mpo humu ndani watu mtakao toa matusi na kashfa mbali
mbali kuhusu mada hii. Lakini huo ndio ukweli, mpende, msipende CHADEMA sasa
limekuwa pango la Mfisadi na wala rushwa, ambao wamekatwa na vyama vyao sasa
wameamia CHADEMA ili wapate nafasi za kuendeleza matakwa yao binafsi. Kwanini
wasubiri kukatwa ndio wakimbilie CHADEMA?????? TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
