Zaidi ya Wapalestina 6000 wako katika jela za Israel

Shirika linalofuatilia masuala ya mateka wa Kipalestina limetoa ripoti mpya inayosema kuwa, zaidi ya Wapalestina 6000 wanaendelea kuteseka katika jela za kuogofya za utawala haramu wa Israel. Qadura Fares, mkuu wa shirika hilo amesema wakati wa kutoa ripoti hiyo kuwa, Wapalestina wanapata mateso makubwa katika jela za Wazayuni na haki zao za kimsingi zinakiukwa.

Baadhi ya wafungwa hao ni watoto walio chini ya umri wa miaka 15. Hii ni katika hali ambayo, utawala haramu wa Kizayuni siku chache zilizopita ulipitisha sheria ya kuwaruhusu askari wake wa magereza kuwalisha kwa nguvu wafungwa wa Kipalestina wanaogoma kula wakilalamikia mateso dhidi yao.

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu pia imezungumzia sheria hiyo kandamizi ya Israel ikisema kuwa, sheria hiyo ni ya kibaguzi na yenye lengo la kuficha mateso ya Wazayuni kwa wafungwa wa Palestina.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia