Staa wa sinema za kibongo,
Elizabeth
Michael ‘Lulu’.
Staa wa sinema za
kibongo, Wema Isaac Sepetu
Habari za mjini zinadai kwamba, Wema amekuwa akishtushwa na
kuchukizwa na kitendo cha Lulu kuwa upande wa aliyewahi kuwa mwandani wake,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kiasi cha kwenda nyumbani kwake, Madale-Tegeta
jijini Dar, usiku wa manane na kujiachia na jamaa huyo anavyotaka.
“Kama mtakumbuka,
kabla ya kifo cha Kanumba (Steven), Wema na Lulu walikuwa ni mashosti kama ilivyokuwa kwa Wema na Snura (Mushi) au Wema na
Kajala (Masanja) au Wema na Aunt (Ezekiel).“Lakini baada ya jamaa (Kanumba)
kuondoka na kisa kizima cha Lulu ndipo Wema akavunja urafiki na Lulu kwa sababu
Kanumba aliwahi kuwa ‘mtu’ wa Wema kama ilivyo
kwa Diamond.
“Ulipita ukimya wa
muda mrefu bila Wema na Lulu kuwa mashosti zaidi ya salamu.
“Lakini mambo yalianza
tena kuwa mabaya baada ya Lulu kumponda Wema alipokuwa akigombea Ubunge wa Viti
Maalum kupitia CCM (Chama Cha Mapinduzi).
“Sasa hivi ishu ni
kitendo cha Lulu kujiachia na Diamond kwenye birthday ya Rome Jones (binamu na DJ wa Diamond) kisha
ile pati ya birthday Diamond kuifanyia nyumbani kwake huku (Lulu) akitupia
picha za mafumbo yaliyoelekezwa kwa Wema.
“Hicho ndicho kinachoendelea
na unaambiwa hali ni tete mno,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa
karibu wa mastaa hao.Baada ya kupata ‘ubuyu’ kamili, Amani lilimtafuta Wema na
kummwagia data ambapo alionesha kushtushwa na kudai kwamba hata yeye anashangaa
ni nini kimetokea.
Kwa upande wake Lulu hakupatikana hewani lakini kwa mujibu
wa mahojiano aliyofanya hivi karibuni juu ya uhusiano wake na Wema, mwanadada
huyo alikiri kuwa rafiki wa Wema kitambo hicho lakini akasema hajui ni nini
kilichotokea zaidi ya kwamba huwa wanasalimiana tu wanapokutana.
Kabla ya mambo kwenda mrama, Lulu na Wema walikuwa mashosti
wakubwa ambapo gazeti hili liliwahi kuwashuhudia wakiwa lokeshi na kulala
pamoja chumba kimoja kama mtu na dada au mtu
na mdogo wake.


