HATIMAYE watu watano wa familia moja waliouawa kinyama kwa
kuchinjwa na watu wasiojulikana wamezikwa kijijini kwao huku vilio vikitawala
eneo la mazishi
Wananchi hao waliyataja mambo saba ambayo wanaamini
yalichangia wabaya wa George kumvamia usiku na kumuua yeye na familia yake.“Kwanza kabisa marehemu alipoanza kuishi eneo lile
alilokutwa na mauti alikuwa kawaida. Halafu akaja akajenga nyumba. Pili
akafungua duka kubwa hapa kijijini.
Tukio hilo
la kinyama lilijiri Septemba 28, mwaka huu saa 9:00 usiku katika Kitongoji cha
Kisesa Kata ya Bugalama Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wakati familia hiyo ikiwa
imelala ndani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemin Mushi alisema chanzo
cha familia hiyo kuuawa kinyama kwa kuchinjwa shingo ni mgogoro wa ardhi madai
ambayo baadhi ya wanakijiji wameyakanusha wakisema si sahihi sana .
Waliouawa katika tukio hilo
ni George Charles (30), Siku John (23) mama wa familia na watoto wao, Mchambi
George (7) Tuma George (5) na Amos George (miezi 9). Wote walizikwa siku moja
katika makaburi ya kijijini hapo.
Uwazi lilifika katika kitongoji hicho na kuzungumza na
baadhi ya wanakijiji, majirani, ndugu na wazazi wa marehemu na kubaini kuwa,
chanzo kinachozungumwa au kuwemo akilini mwa watu ni wivu wa maendeleo ya
familia hiyo.
Baadhi ya wananchi ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini wakiwemo watu wa karibu na familia hiyo,
walisema chanzo ambacho kinaweza kusababisha tukio hilo
ni kujituma sana
kwa marehemu George hivyo kuwazidi kiuchumi wananchi wengine wa kijijini hapo.
“Tatu, marehemu alikuwa na roho nzuri. Anakopesha kila mtu.
Lakini nne ni jinsi duka lake
lilivyokuwa limejaza
bidhaa nyingi kupita maduka mengine. Duka lake lilikuwa
na kila kitu.“Tano, nyumba ya marehemu George ndiyo iliyokuwa na umeme hapa
kijijini tena wa sola. Kwake mwanga usiku ulitofautisha nyumba yake na
nyingine. Lakini jambo la sita ni jinsi maisha yake na familia yalivyokuwa ya
amani. Hilo
nalo naamini liliwaumiza wabaya wake.
“Saba, yule bwana mauzo ya duka lake kwa
siku yaliwazidi wafanyabiashara wengine wote. Kwa hiyo alikuwa akikata mbuga
kuelekea kweye mafanikio zaidi. Naamini wabaya wake walipoyaangalia haya
wakaona dawa yake ni kuimaliza hii familia,” alisema mwanakijiji huyo.
Kauli hiyo ilionekana kuungwa mkono na mjomba wa marehemu,
Renatus Dutu kwa maelezo kuwa kutokana na maendeleo yake marehemu, inawezekana
baadhi ya wanakijiji walikuwa hawayataki.“Nyumba yake ndiyo ilikuwa na umeme tu
hapa kijijini. Alikuwa akichaji simu nyingi za wananchi. Duka lake lilikuwa
kubwa. Tuna wasiwasi kwamba uwezo wake unaweza kuwa chanzo,” alisema Dutu.
Portini Shili ni jirani wa familia iliyochinjwa ambapo
anaeleza kuwa, chanzo hicho cha mgogoro wa ardhi hakikubaliki na wanakijiji
bali maendeleo ya familia hiyo kiuchumi ndiyo yanasemwa kuchangia.
“Hilo
eneo la ardhi wanaloeleza polisi lilikuwa ni la mpwa wangu (mtoto wa dada
yake). Wakati wanauziana eneo hilo
mimi nilikuwepo. Aliuziwa na baba wa kambo wa marehemu (George) lakini wakati
ananunua eneo hilo
tayari familia ya George ilikuwa ikiishi humo mpaka vifo,” alisema.
“Hakuna ukweli juu ya chanzo hiki cha mgogoro wa ardhi na
baba wa kambo ambaye anatuhumiwa na amekamatwa ni mzee mwenye heshima hapa
kijijini lakini hatuwezi kusema sana ,
sheria inachunguza. Mimi nilikuwa ndani ya familia hiyo, mapenzi ya mzee huyo
kwa mtoto wake (George) yalikuwa makubwa sana
kutokana na kuwasaidia,” alisema Shili.
Mbali na jirani huyo, baba mzazi wa mama wa familia, John
Lutamba, ndugu wa marehemu (Zengwe Sendama, mjomba (Renatus Dutu) nao walieleza
kuwa hawaamini sana kama chanzo cha vifo ni mgogoro wa ardhi kwa vile hakukuwa
na mgogoro wowote katika familia hizo.
“Hakuna ukweli wa juu ya chanzo hicho mpaka sasa tupo
tunajiuliza nini chanzo na wahusika ni akina nani? Na hakuna mwenye jibu katika
familia yetu, hakuna mgogoro wowote wa ardhi na tulikuwa tunaishi vizuri,”
alisema Lutamba.
Akizungumza na Uwazi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bugalama,
Christopher Kulwa alisema tangu amekuwa kiongozi katika eneo hilo hajawahi kusikia au kuletewa ugomvi au
mgogoro juu ya familia hiyo.
Alisema kama uongozi wa serikali ya kijiji bado unafuatilia
chanzo na wahusika wa tukio hilo
ambapo alisema katika hatua za awali za uchunguzi waliamua kila mwana kijiji
kupiga kura ya siri.
“Tumeendesha kura ya siri kwa kila mtu ambaye anaweza
kuwafahamu wahusika na chanzo. Kura hiyo
tayari tumepatiwa baadhi ya majina ya watu ambao walihisiwa kuhusika,
tunayafanyia kazi kwa kushirikiana na jeshi la polisi,” alisema mwenyekiti
huyo.
Kamanda Mushi alisema kufuatia mauaji hayo jeshi lake linawashikilia
watu watatu ambao ni Migata Lusalago (50), Jihelya Migata (30) na Sollo Kengele
(31) wote wakazi wa kijiji hicho.