Mbeya. Watoto wawili wa familia moja wameteketea kwa moto huku mama yao akiungua sehemu kubwa ya mwili wake baada ya chumba walichokuwa wamelala kuungua kwa moto katika Mtaa wa Itiji jijini hapa usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya , Ahmed Msangi amewataja
watoto waliofariki kuwa ni Raymond
Erasto na Nestory Erasto (6) na kwamba mama yao aliyejeruhiwa ni Happy Erasto
(26).
“Tukio hilo limetokea
usiku wa kuamkia leo baada ya kibatari cha moto kuangukia godoro wakati watu
wakiwa kwenye uzisingizi,” amesema kamanda Msangi
Kamanda Msangi amesema mama wa watoto walioteketea kwa moto,
alijeruhiwa baada ya kujitosa kwenye moto ili awaokoe watoto wake na kwamba kwa
bahati mbaya hakufanikiwa.
Tukio la watu kuungua mkoani Mbeya ni la pili baada ya
mwishoni mwa mwezi Septemba kutokea tukio lingine wilayani Chunya ambapo mtoto
Elizabeth Mwalupembe aliteketea kwa moto baada ya nyumba alimolala kuungua.
