Vitambulisho 134 vya Kupigia kura, vimekamatwa na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa –TAKUKURU- mkoani Kagera baada ya kukutwa
vimenunuliwa na Kundi la watu kutoka kwa wapiga kura.
Taarifa ambazo zimethibitishwa na Naibu mkuu wa Takukuru
mkoani Kagera, John Joseph vitambulisho hivyo vimekamatwa vikiwa tayari
vimenunuliwa kutoka kwa wananchi kwa bei ya kati ya shilingi 5,000 hadi 10,000.
Amesema kuwa kukamatwa kwa Vitambulisho hivyo, kumetokana na
baadhi ya Vijana walioshawishiwa kuuza kadi hizo na kundi la watu wanaopita,
kutoafiki na kisha kulazimishwa kufanya hivyo
