ACT Wazalendo yateua wasomi kuongoza kamati

Kamati Kuu ya Chama cha Wazalendo (ACT-Wazalendo) imeidhinisha uteuzi wa Wenyeviti na Makatibu wa Kamati za Kitaifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Naibu Katibu Mkuu, Msafiri Mtemelwa, Mustapha Akonaay (63) anakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uadilifu,Ulinzi na Usalama wa Chama.

Ilisema  Akonaay ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Stashahada ya Sheria kutoka kilichokuwa Chuo cha Maendeleo Mzumbe.

Ilisema kamati Kuu imempitisha pia  Yeremiah Kulwa (48) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa
Ilisema  Yeremiah Kulwa  ana Shahada ya Uzamili katika Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe na Shahada ya kwanza ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini.

Taarifa hiyo ilimtaja  Mosses Machali  (34) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo na Uchaguzi na kwamba  Machali ana Shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Jamii na Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu John (St. John’s) na Shahada ya kwanza katika Sayansi ya Jamii na Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT).

Ilisema Albert Msando  (36) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje na kwamba ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni Wakili wa Kujitegemea wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Ilimtaja  Carol  Ndosi (32) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma na kwamba anajulikana katika tasnia ya habari nchini Tanzania
na  amefanya kazi katika tasnia ya habari na masoko na ana Shahada ya kwanza katika tasnia ya Amani na Utatuzi wa Migogoro kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala.

Taarifa hiyo ilimtaja  Venance Msebo (32) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Miradi ya Kujitegemea na ana Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Diploma ya Juu katika Kodi kutoka Chuo cha Kodi.

Ilimtaja  Mhonga Ruhwanya (37) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamaii na ana Shahada ya Uzamili katika Maendeleo ya Jamii na Uchumi kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Shahada ya Kwanza katika Sosholojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ilimtaja  Theopista Kumwenda (29) kama Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje na kwamba ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT).

Wengine ni Ado Shaibu (32) ambaye amekuwa Katibu wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma na ana Shahada ya kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyohitimu Mwaka 2015 na Dorothy Temu (40) ambaye amekuwa Katibu wa Kamati ya Utafiti, Sera na Mipango akiwa na Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Fiziotherapi (MSc Physiotherapy) na Shahada ya Kwanza katika eneo hili (BSc Physiotherapy) kutoka katika Chuo Kikuu cha Western Cape nchini Afrika Kusini.

Emmanuel Thomas(27) amekuwa Katibu wa Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje na ana Shahada ya kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe na ni Wakili wa Kujitegemea wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Mhandishi Mohamed Mshamu (44) amekuwa Katibu wa Kamati ya Uadilifu, Ulinzi na Usalama wa Chama na ni  Mhandisi kitaaluma mwenye Shahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Uhandisi na Shahada ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mchange Habibu (30) ameteuliwa kuwa Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa na  kabla alikuwa Katibu wa Mipango na Mikakati wa chama hicho akiwa na Shahada ya Kwanza katika Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Mohammed Massaga (42) amekuwa Katibu Kamati ya Mafunzo na Uchaguzi na kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu wa Kamati ya Chaguzi na Kampeni ya ACT-Wazalendo na ana ana Stashahada ya Uandishi wa Habari kutoka Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Janeth Joel (42) ameteuliwa kuwa Katibu wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii (Bara) na ana Stashahada katika Theolojia na Maarifa ya Biblia.

Seif Hamad Suleiman  (25) ameteuliwa kuwa Katibu Msaidizi Itikadi, Mawasiliano na Uenezi (Zanzibar) na ana Stashahada katika Utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka kutoka Chuo cha Utawala wa Umma (IPA) Zanzibar.
Mpya zaidi Nzee zaidi