Aliyekuwa Mchekeshaji maarufu kutoka kundi la Vituko Show, Ismail Makombe maarufu Baba Kundambanda wakati wa uhai wake
Pia, Kundambanda aliyekuwa mwanasiasa aligombea ubunge wa Jimbo la Masasi mkoani Mtwara kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mkuu 2015.
Naibu Katibu mkuu wa CUF Tanzania Bara, Shaweji Mketo alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba, Kundambanda ameacha pengo kubwa kwao.
Wakati wa uhai wake, Kundambanda pia, alikuwa mtunzi wa nyimbo za kuhamasisha harakati mbalimbali za jamii.