F SMAUJATA Kanda ya Kaskazini yaimarisha ushirikiano na Serikali wilayani Mbulu | Muungwana BLOG

SMAUJATA Kanda ya Kaskazini yaimarisha ushirikiano na Serikali wilayani Mbulu



Na John Walter -Mbulu

Leo tarehe 26 Agosti 2025, Katibu wa SMAUJATA Kanda ya Kaskazini, Shujaa Ezekiel Tlanka, amefanya ziara katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kwa lengo la kuimarisha uhusiano na viongozi wa serikali katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Tlanka alikutana na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mheshimiwa Michael Semindu ambapo alimpongeza kwa juhudi za kuwasimamia wananchi na kusimama mstari wa mbele kupinga vitendo vya ukatili. 

Aidha, amesisitiza kuwa SMAUJATA inatambua mchango wa viongozi wa serikali katika ngazi zote za utawala.

Baada ya mazungumzo hayo, Katibu huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbulu pamoja na Mkuu wa Upelelezi Wilaya na Kiongozi wa Dawati la Jinsia na Watoto ambapo amelishukuru Jeshi la Polisi nchini kwa ushirikiano wao wa hali na mali, mchana na usiku, katika kupambana na wahalifu wanaojihusisha na ukatili na kuhakikisha kesi zinapelekwa mahakamani ili haki itolewe. 

Tlanka amebainisha kuwa ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za SMAUJATA Kanda ya Kaskazini kuimarisha utendaji wa majukumu ya pamoja kati ya serikali na jumuiya hiyo, kuhakikisha jamii inalindwa dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Katibu wa SMAUJATA alipokelewa na viongozi wa jumuiya hiyo wilayani Mbulu.


Picha za pamoja 







Post a Comment

0 Comments