AJALI: Basi la Barcelona lauwa watu 10

Watu 10 wamefariki dunia na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la Barcelona lililokuwa linatoka Dar es Salaam kuelekea Mtwara leo (Jumatatu) asubuhi, kuanguka katika eneo la Miteja mkoani Lindi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga amesema waliopoteza maisha ni wanawake sita, mwanamume mmoja na watoto watatu.

Alisema wanawake wamejeruhiwa 16, wanaume 18, watoto watatu wa kike na saba wa kiume.

Kamanda Mzinga alisema chanzo cha ajali hiyo ni tairi la mbele la basi hilo kupasuka hivyo kusababisha dereva kupoteza mwelekeo.

Hata hivyo, alisema uchunguzi umebaini pia kuwa basi hilo lilikuwa na abiria kupita kiasi kinachotakiwa.

“Abiria walikuwa 54 wakati basi lina uwezo wa kubeba abiria 48. Abiria sita walizidi. Hilo ni kosa la usalama barabarani,” alisema.

Alisema polisi wanamsaka dereva wa basi hilo.


Angalia Picha za Ajali..









Mpya zaidi Nzee zaidi