Naibu Meya, mtendaji wasomewa mashtaka

ALIYEKUWA Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe (Chadema) na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Daraja Mbili, Modestusi Lupogo,
jana walisomewa maelezo ya awali katika kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


Msofe na Lupogo wanadaiwa kujipatia Sh. milioni nane zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya mradi wa usambazaji wa maji.

Msofe, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Daraja Mbili na mwenzake, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Arusha, na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Augustine Rwizile.

Wakili wa Takukuru, Hamidu Simbano, alidai mahakamani hapo kuwa Msofe akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya
Kata na Lupogo akiwa Katibu, Mei 13, 2013, wakiwa katika kikao walikubaliana kuomba kiasi Sh. milioni 15 kutoka Halmashauri ya jiji kwa ajili ya mradi wa usambazaji wa maji katika mitaa ya Alinyanya na Sanare.

Source: Nipashe
Mpya zaidi Nzee zaidi