Njaa yazikumba wilaya 42 nchini

Wakati baa la njaa na ukame likiendelea kuukumba Mkoa wa Kagera, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mifugo, Florence Turuka amesema  kuna wilaya 42 nchini zinazokabiliwa na uhaba wa chakula uliosababishwa na ukame.

Ukame huo umesababisha pia ng’ombe waliokuwa wanauzwa kwa Sh 600,000 wilayani Karagwe mkoani Kagera kuuzwa kwa Sh 20,000.

Wilaya zinazokabiliwa na tatizo hilo ni za mikoa ya Tanga, Singida, Mara, Dodoma, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.
Mpya zaidi Nzee zaidi