
Wakati mwenyekiti wa chama cha wananchi cuf Prof. Ibrahimu Lipumba anayetambulika na msajili wa vyama vya siasa akitafuta suluhuhisho la mgogoro unaokikabili chama hicho,wajumbe wa baraza kuu na wabunge wa CUF wamesema hawapo tayari kukaa meza moja na kumaliza tofauti zao wakidai kuwa Prof. Lipumba alikataa maridhiano wakati wakimuomba asijiudhuru.
Prof. Ibrahimu Lipumba akiwa ziarani mikoa ya kanda ya kusini inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara amewaomba wafuasi na wanachama wa chama cha wananchi cuf kupitia dini zao kukiombea chama chao ili kiweze kumaliza tofauti zao na kuanza kukiimarisha chama
Wakati Prof. Lipumba lipumba anaomba maridhiano wajumbe wa baraza kuu na wabunge wa cuf mikoa ya lindi na Mtwara wanasema kwa kuzingatia katiba ya chama,hawako tayari kukaa meza moja na badala yake wanafuata katiba.