F 22 wakamatwa Dar wakihusishwa na matukio ya uporaji wa silaha | Muungwana BLOG

22 wakamatwa Dar wakihusishwa na matukio ya uporaji wa silaha

Kikosi cha polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam cha kupambana na wizi wa kutumia silaha na nguvu, kimefanikiwa kukamata watuhumiwa 22 wanaohusika na matukio ya uporaji wa kutumia silaha kwenye magari na mitaani.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema watuhumiwa hao walio na umri kati miaka 18 na 19 wamekuwa wakijikusanya katika vikundi kufanya vitendo vya uporaji wakati wakati wa foleni pamoja na wengine kujigawa katika foleni ili kutekeleza uhalifu huo.

“Tarehe 11 mwezi wa 12,2016 huko Temeke maeneo ya Keko Magulumbasi na mtaa wa Veta na Chango’mbe hasa yale mataa ya Chango’mbe na Veta askari walifanikiwa kuwakamata watu wapatao 10 lakini maeneo mengine ya Kinondoni maeneo ya Ilala wapatao watu 12 wakiongozwa na mtuhumiwa mmoja maarufu anaitwa Ayubu Amir (19) mkazi wa Mtoni Mtongani pamoja na Shabani Fadhili (18) mkazi wa Keko Toroli hawa ni vibaka,” alisema Kamanda Sirro.

“Tena hawa ni vibaka sugu lakini mnaweza mkaangalia ni watoto wadogo ni miaka 19 na miaka 18 ndo ile lugha huwa nasema wazazi hasa mama tujitahidi sana kutunza watoto wetu,” aliongeza.