Kipindupindu chatikisa Dodoma, chaua wawili wengine walazwa

WATU wawili wamefariki dunia na wengine nane wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme, akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema watu hao walifariki dunia wiki iliyopita baada ya kuugua ugonjwa huo, wakati nane wanaendelea kupata matibabu.

“Kutokana na kuingia kwa ugonjwa huu wa kipindupindu katika manipsaa yetu, tunatakiwa tuzingatie kanuni za usafi kwani maambukizi yanaenea kwa haraka ,” alionya Mndeme.

Mndeme alisema walianzisha kampeni maalumu ya kuondoa ugonjwa huo ambao iwapo utadhibitiwa mapema hautaleta madhara zaidi.

Source: Nipashe
Mpya zaidi Nzee zaidi