Dar es Salaam. Mamilioni ya watu duniani hujiwekea malengo kila wanapouanza mwaka. Wapo ambao wanayafanikisha, lakini wengine huishia njiani. Inakadiriwa kuwa katika kila watu milioni moja ambao huweka malengo, nusu yake huwa wanayasahau ifikapo Machi.
Zipo njia mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia kufanikisha malengo uliyojiwekea. Miongoni mwa njia hizo ni matumizi ya fedha zako lazima yaanzie kwenye maandishi.
Mafanikio yoyote yanayoonekana leo yalifanyika katika muda sahihi.
Siku zote unapotarajia kufanya jambo weka mpango au ikibidi kuwa na mipango mbadala iwapo ule wa awali hautakwenda kama ulivyotarajia.
Unapotaka kujiendeleza kielimu, kufanya kazi au kufungua biashara ni vyema ukafanya utafiti ili kujua kwa undani.
Binadamu anapitia zama ngumu; kutopoteza mwelekeo katika dunia inayoendeshwa na teknolojia, taarifa pomoni, kazi nyingi, majukumu ya familia na mengine mengi, lakini kubaki katika mstari ndiyo njia pekee itakayofanikisha safari lyako ya mafanikio katika kazi au biashara.
Afya ni mtaji. Afya ni utajiri. Unaweza kutimiza majukumu yako kwa urahisi pale unapofanya kazi zako bila kuhitaji usaidizi kutokana na kuzorota kwa afya.
Mafanikio huja kwa urahisi pale unapokuwa umezungukwa na watu sahihi. Watazame marafiki zako wanaokuzunguka. Je, wanachangia mafanikio au anguko lako?
Kusoma vitabu, majarida, kutazama filamu, kusikiliza muziki na kusafiri ni namna mojawapo wa kukukuza kimaarifa.
Lolote linaweza kutokea kabla ndoto haijawa halisi kwa maana hiyo ni vizuri kuwa tayari.
Unaposhindwa jambo usitafute sababu ya kujitoa badala yake tafuta njia mbadala ya kuhakikisha kazi hiyo inafanikiwa.