Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Yusuph Masaun amepiga marufuku ununuzi wa sare za jeshi la zima moto na uhamiaji kwa taasisi binafsi na badala yake ameagiza sare hizo zizalishwe katika viwanda vya jeshi la magereza nchini.
“Kuanzia leo uhamiaji zima moto wote washone nguo, kama ambapo magereza wanashona katika kile kiwanda, kwamba dhamira ya mheshimiwa rais ya kutoa maelekezo ambayo yamefuatilia utendaji kazi wake nimeridhika, kwamba ni marufuku kama alivyosema mheshimiwa rais kwa askari Magereza na askari wote wa vyombo vya usalama nchini kununua uniform kwa raia, jeshi la magereza linatengeza furniture zenye ubora wa hali ya juu,” alisema Mhandisi Masauni.
