Uongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) umewataka wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kuhakikisha mawakala wa vyama vya siasa wanakula kiapo cha kutunza siri kwa mujibu wa matakwa ya kanuni za uchaguzi.
Agizo hilo limetolewa mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya uchaguzi, Bw. Ramadhani Kahilima wakati alipokuwa akifungua mafunzo kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi, ambao wataendesha zoezi la uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani Zanzibar na kata mbalimbali zisizo na madiwani.
Aidha, kiongozi huyo wa Tume ya taifa ya uchaguzi alichukua wasaa huo kuwahasa wasimamizi hao wa uchaguzi kuhakikisha wanafuata, taratibu, sheria na kanuni zilizopo, ili chaguzi watakazozisimamia ziendeshwe kwa uhuru na haki.
Chaguzi ndogo zilizotangazwa na Tume ya taifa ya uchaguzi, zinatarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu katika kata 22 na jimbo moja la uchaguzi, ambalo ni jimbo la Dimani Zanzibar.