Mfanyabiashara mashuhuri nchini Zimbabwe, Wicknell Chivayo, pamoja na mke wake Lucy "Lulu" Muteke, wamethibitishwa kufariki dunia baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo la Marondera, mashariki mwa mji mkuu wa Harare.
Aidha taarifa za vifo vya wanandoa hao zamethibitishwa na msemaji wa familia, Herbert Chivayo.
Jeshi la Polisi la Zimbabwe (ZRP) limeeleza kuwa watu wote sita waliokuwa ndani ya helikopta hiyo wamepoteza maisha, wakiwemo marubani wawili na abiria wengine wawili ambao majina yao bado hayajatangazwa.
Msemaji wa Serikali, Nick Mangwana, amebainisha kuwa miili ya marehemu iliharibika vibaya kwa moto, na taratibu za kiuchunguzi zinaendelea ili kuwatambua kikamilifu wahanga hao kabla ya kutoa taarifa rasmi kwa umma.
