Nyumba nane na mali za wakazi zimeteketezwa kwa moto katika vurugu zinazodaiwa kusababishwa na mgogoro wa ardhi

Nyumba nane na mali za wakazi wa Kitongoji cha BWENGOMA kata ya KAKUNYU wilayani Misenyi mkoani Kagera zimeteketezwa kwa moto na baadhi ya wanachi kujeruhiwa vibaya katika vurugu zinazodaiwa kusababishwa na mgogoro wa ardhi kati ya mwekezaji wa ufugaji na wakazi wa kijiji hicho.

Mwandishi wa habari hizi amefika katika eneo hilo, na kujionea nyumba zilizochomwa moto na na kushuhudia moja kwa moja vurugu kati ya wananchi na walinzi wanaodaiwa ni wa mwekezaji mwenye kitalu namba 20, ambapo mwananchi mmoja alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Wakiongea nje ya nyumba zilizochomwa moto wamedai uwa mgogoro huo unasababisha na mwekezaji katika kitalu no 20, ambapo kuna makazi yao akiwataka wahame kwa kuwa amepewa na serikali eneo hilo kulitumia kwa ajili ya ufugaji wa kisasa, ili hali kuna mazao yao na makazi yao ya kudumu huku wakiitwa si Raia wa Tanzania.

Viongozi wa Serikali katika eneo hilo wamesema kuwa wametoa taarifa kwa ngazi ya kata na wilaya, juu ya kuwanusuru wananchi hao na madhira wanayofanyiwa na mwekezaji, lakini wanashangaa kuona hawapati msaada wa ulinzi au kuwakamata anaochoma nyumba zao.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Misenyi Luteni kanali Denis Mwila, hakupatikana ofisini kwake kuongelea hali hiyo lakini akihojiwa kwa simu amesema kuwa kilichopo katika kijiji hicho siyo mgogoro, bali ni baadhi ya wafugaji kuvamia isivyo halali eneo la mwekezaji wa ufugaji, ambaye amepata eneo hilo kisheria.
Mpya zaidi Nzee zaidi