Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali itapambana na janga la dawa za kulevya kwa dhati bila kumuonea mtu yeyote na kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki.
Ametoa kauli hiyo Ijumaa hii bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa sita wa Bunge la 11.
Alisema, “Lengo la Serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri kwa maana ya wauzaji na wasambazaji. Dhamira ya Serikali ni kupambana na janga hili kwa dhahiri na kwa dhati bila kumuonea mtu yeyote na kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki.”
Aidha waziri Mkuu alizungumzia idadi ya watu ambao hadi sasa wamekwishakamatwa katika nchi mbalimbali. amesema takwimu za jumla zinaonyesha kuwa Watanzania 515 wamekamatwa na kufungwa gerezani kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. “Nchini China Watanzania walioko magerezani ni zaidi ya 200, Brazil kuna Watanzania 12, Iran wako Watanzania 63, Ethiopia Watanzania 7 na Afrika Kusini wako Watanzania 296.”
Waziri Mkuu amesema moja ya hoja za Kamati za Kudumu za Bunge iliyojadiliwa na kuibua hisia kali katika mkutano huu wa Bunge ni kuhusu vita inayoendelea nchini dhidi ya dawa za kulevya na akawaomba Watanzania wote waiunge mkono Serikali juu ya vita hiyo.
Alisisitiza, “Watanzania wote ni mashahidi kwamba vijana wetu wengi wameendelea kudhoofika kiafya kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Dawa za kulevya ni hatari sana kwa usalama na ustawi wa Taifa letu. Vita hii inayopiganwa sasa dhidi ya uagizaji, uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa. Sote tunapaswa kuunga mkono jitihada hizo.”
Amesema dawa hizo za kulevya, huingia zaidi kutumia njia za bandari bubu kupitia Bahari ya Hindi na mipakani kwa njia ya magari binafsi au mabasi kupitia nchi za Kenya, Uganda na Mpaka wa Tunduma.
Waziri Mkuu aliyataja madhara ya kiafya yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya kuwa ni pamoja na kuathirika kwa mfumo wa fahamu kwa mtumiaji ikiwamo kuchanganyikiwa, kuwa na ulevi usioponyeka kirahisi na kusababisha kifo kama mtumiaji atazidisha matumizi ya dawa za kulevya
“Madhara ya kiuchumi ni pamoja na gharama kubwa za kuwatibu waathirika wa dawa za kulevya, gharama kubwa za uchunguzi wa kimaabara kwenye Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na watumiaji wa dawa za kulevya kushindwa kujisimamia na kuendesha maisha yao.”
Bunge limeahirishwa hadi Jumanne, Aprili 4, 2017.