Zaidi ya wakazi elfu mbili kutoka katika vijiji vitatu vilivyopo kata ya Kwihancha wilayani Tarime mkoani Mara wanatarajia kuondokana na adha ya kutembea umbali wa saa tatu huku wakiwa na mifugo yao kwa ajili ya kutafuta maji baada ya kuzinduliwa kwa mradi mkubwa wa bwawa la maji litakaokuwa likihudumia wakazi wa kata hiyo na maeneo mengine ya jirani.
Mradi huo ambao utakuwa na manufaa kwa wakazi wa maeneo hayo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 74 mpaka kukamilika kwake na unatajwa kuwa na manufaa kwa binadamu na mifugo.
Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo uliojengwa na shirika la hifadhi ya taifa ya tanapa kwa kushirikiana na nguvu za wananchi mkuu wa wilaya ya Tarime Bw. GLORIUS LUOGA amesema kukamilika kwa mradi huo sasa unakuwa chachu ya kusaidia kusukuma mbele maendeleo ya wananchi hao ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitumia muda mwingi kwaajili ya kusaka maji.
Wananchi nao wakaelezea namna walivyoupokea mradi huo.