Kaimu mkurugenzi mtendaji wa bohari kuu ya dawa-MSD- Bwana Cosmas Aron Mwaifwani na kaimu meneja manunuzi wa MSD, Frederick Rubanga Nicolaus wamepandishwa kizimbani katika mahakamani ya hakimu mkazi Kisutu kujibu shtaka la matumizi mabaya ya madaraka.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu Respicius Mwinjage mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa-TAKUKURU- Aneth Mavika amedai kuwa kati ya machi mosi na 19,2013 washtakiwa wakiwa makao makuu ya bohari kuu ya dawa yaliyopo Temeke kwa nafasi zao walitumia madaraka yao vibaya kwa kuandaa,kusaini mkataba namba moja na kuisababishia kampuni ya H.H Hillal and Company Limited kupata manufaa ya shilingi milioni 482.266.000.
Baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa wote wamekana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi umekamilika ambapo Washtakiwa wametakiwa kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika ambao wamesaini bondi ya sh 20 milioni na mshtakiwa kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya sh 200 milioni hatua ambayo wamekamilisha na kuachiwa huru,kesi hiyo imeahirishwa hadi machi 21 mwaka huu ambapo washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali.
Katika hatua nyingine mbunge wa singida mashariki mhe. Tundu lissu aliyekuwa na akikabiliwa mashtaka manne ya uchochezi katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu amefutiwa mashtaka hayo na kuachiwa huru na kisha kukamatwa tena na kupelekwa polisi.
Maamuzi ya kuachiwa huru na mahakama yamekuja baada ya upande wa mshtaka ukiongozwa na wakili wa serikali paul kaduchi kuiomba mahakama kumwachia huru chini ya kifungu cha 91(1) cha mwenedo wa makosa ya jinai ambacho kimesema mkurugenzi wa mashtaka ana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yake.
Baada ya kutoa taarifa hiyo mahakama imekubaliana na maamuzi hayo na kumwachia huru ambapo alipotoka nje ya jengo la mhakama alikamtwa tena na kupelekwa polisi, kifungu cha 91 kinampa nguvu mkurugenzi wa mashtaka kumwachia huru mshtakiwa na kisha kinampa mamlaka ya kumakamata na kuendelea na uchunguzi muda wowote.
Jeshi la polisi limemwachia kwa dhamana mhe. Tundu lissu ambapo anatakiwa kufika kituo cha polisi machi 13 mwaka huu.
Aidha anakabiliwa na tuhuma za kutoa maeneo ya uchochezi ambayo yangeweza kuleta mtafuruku wa kidini katika jamii alipohutubia kamepni za uchaguzi mdogo jimbo la dimani zanzibar mwezi januari mwaka huu.
Chakufanya ni Kubofya Link hapo chini na Ufate Maelekezo ya Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..
Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako... USIWE NA WASIWASI HUDUMA HII NI SALAMA KABISA..

***********
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote, Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ... Chakufanya ni Kubofya Link hapo chini na Ufate Maelekezo ya Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..