Raia wanne wa Burundi waliomaliza kifungo chao kumrejesha kwao


Raia wanne wa Burundi wamemaliza kifungo chao leo, Oktoba 13, 2026, Mkoani Kigoma na wanatarajiwa kurejeshwa nchini mwao kwa mujibu wa sheria na taratibu za Uhamiaji.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa kifungo chao, Mkuu wa Kanda Maalumu ya Kigoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji SACI Dismas Mlula, amewataka raia hao kuwa raia wema na kuzingatia sheria na taratibu za Uhamiaji pindi watakapohitaji kuingia nchini Tanzania.

Aidha, SACI Mlula amesisitiza kuwa Ofisi ya Uhamiaji Kanda Maalumu ya Kigoma inaendelea kutoa elimu kwa umma kupitia kampeni ya “Mjue Jirani Yako,” inayolenga kuhamasisha wananchi kufahamu majirani zao na kuzingatia sheria na taratibu za Uhamiaji..

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi