Bibi wa miaka 78 jela miaka 30 Kwa bangi kilo 33.25


Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza imemhukumu Suzana Marwa, maarufu kama Maswi (78), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kukutwa na bangi yenye uzito wa kilogramu 33.25.

Suzana alikamatwa Machi 29, 2026 katika eneo la Bugarika Kaskazini, baada ya maafisa wa DCEA kufanya upekuzi nyumbani kwake na kukamata bangi iliyokuwa kwenye mifuko miwili na ndoo ya plastiki.

Katika hukumu iliyotolewa Septemba 23, 2026, Hakimu Mkazi Mwandamizi Clement Tuji alieleza kuwa umri mkubwa wa Suzana ungestahili kuzingatiwa katika kumpunguzia adhabu, lakini sheria inaweka kifungo cha lazima cha miaka 30.

Mahakama pia iliamuru bangi hiyo iteketezwe na fedha taslimu Sh195,000 zilizokamatwa zitaifishwe

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi