F Chirwa: Huwezi kuitoa Yanga kwenye mbio za ubingwa VPL | Muungwana BLOG

Chirwa: Huwezi kuitoa Yanga kwenye mbio za ubingwa VPL


STRAIKA wa Yanga Obrey Chirwa amesema bado wana nafasi ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa bado wataendelea kupambana vizuri kwenye mechi zijazo ili kupata matokeo mazuri.

Chirwa ambae kwasasa amekuwa na msaada mkubwa katika kikosi cha Kocha mkuu George Lwandamina, huku akiwa amepachika magoli nane katika ligi kuu  tangu alipo sajiliwa na  Yanga akitokea Platinum ya Zimbabwe.

Chirwa amesema “Huwezi kututoa kwenye mbio za ubingwa kwa mechi mbili ambazo kwetu tumeambulia alama moja.

“Mimi bado naamini tukishikamana vizuri kuanzia viongozi hadi wachezaji nina imani kombe linabaki mitaa ya Jagwani,” alisema Chirwa.

Nyota huyo ambae  usajili wake ulizua gumzo kwa mashabiki  hadi kwa wazee wa Yanga kama (mzee Akilimali) huku wakimuona hafai amesema penati aliyokosa Msuva ilisababishwa na uwanja kuwa mbovu.




Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote, Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ... 

Chakufanya ni Kubofya Link hapo chini na Ufate Maelekezo ya Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako... USIWE NA WASIWASI HUDUMA HII NI SALAMA KABISA..