Moto mkubwa wazuka katika msitu mmoja nchini Kenya

Siku ya Ijumaa majira ya jioni moto mkubwa ulivamia msitu maarufu wa Menengai na kuteketeza eneo la ardhi ya zaidi ya ekari 200.

Polisi na timu ya wataalamu wa wazima moto walifika eneo hilo linalopatikana katika bonde maarufu la Rift Valley .

Mkuu wa idara ya huduma ya misitu nchini Kenya David Mtoro alifahamisha kuwa wazima moto wanaendelea na juhudi ya kuzima moto huo huku pia miti kadha ya asili ikiripotiwa kuharibika .

Msitu wa Menengai ni makao  ya aina 169 ya mimea mbali mbali ,wanyama pori na ndege walio katika hatari ya kupotea au hata vigumu kupatikana mahali kwingine .

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana .
Mpya zaidi Nzee zaidi