Huu ndio ujumbe wa Serena William kwa Kijacho wake

 Mcheza tennis namba moja duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams, ambaye alituonesha ujauzito wa wiki 20 kupitia Snapchat yake, Sasa amedhihirisha kuwa yeye ni mama kijacho kweli.
Serena, ambaye kwa sasa yupo katika mahusiano na Alexis Ohanian, amemuandika ujumbe mfupi kwa unborn wake kupitia Instagram yake. Huku akiudhuhirishia umma na dunia kuwa anafurahia hali yake ya sasa na ikimpa nguvu.

Mashabiki wa tennis kwa sasa watakuwa na amani, kwani Serena amelieleza jarida la ‘The New Your Times’ Kelly Bush Novak, kuwa kwa sasa anapumzika ila baada ya kujifungua, atarejea dimbani.

Hii sio mara ya kwanza mastaa duniani kuandika ujumbe kwa watoto wao watarajiwa. Bongo tuliona Idriss Sultan pia aliwahi kuandika ujumbe kwa watoto wake na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, ingawa hayo yaliishia kwingine.
Mpya zaidi Nzee zaidi