Kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu ni rufaa ya Simba Kwa Bodi ya ligi wakidai wapewe pointi za mchezo dhidi ya Kagera sugar uliochezwa Jumapili iliyopita na Simba kufungwa Kwa magoli 2-1. Simba walimkatia rufaa mchezaji Mohamed Fakhi wa kagera Sugar wakidai alicheza akiwa na kadi tatu za njano na hivyo Kagera kukiuka taratibu na kanuni za ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
Kamati ya Masaa 72 imetoa ufafanuzi kuwa Maamuzi ya rufaa ya Simba dhidi ya Mohamed Fakhi yatatolewa Alhamisi ya wiki Ijayo.
