Tottenham yampata Messi


Kocha Mauricio Pochettino amemtaja mshambuliaji wake, Harry Kane kuwa ndiye Lionel Messi wa Tottenham. Mchezaji huyo anayejiandaa kurudi uwanjani baada ya kupona majeraha yake, amekuwa kivutio kwa kocha huyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England, ameamua kurudi uwanjani baada ya kuwa nje kutokana na kuumia enka wakati timu yake ilipokutana na Watford wiki iliyopita.
Kane aliifungia timu yake mabao 19 katika Ligi Kuu England msimu huu, huku akiiwezesha timu yake kujiimarisha katika nafasi ya pili, huku ikiwa nyuma kwa pointi saba kabla ya michezo ya jana.

Pochettino anaamini kwamba Kane ni mchezaji mwenye kipaji cha pekee katika kikosi hicho, hivyo kufikia hatua ya kumlinganisha na Messi ambaye anakipiga La Liga kwenye klabu ya Barcelona inayoongoza ligi hiyo.

Kocha huyo alisema ni jambo la ajabu kuhoji kuhusu umuhimu wa Kane mwenye miaka 23.

Pochettino alisema, “Sina wasiwasi na kiwango cha Harry Kane. Hata akicheza kuanzia mwanzo wa mchezo au akiingia kipindi cha pili sina shaka naye bado amekuwa mchezaji bora. Katika kikosi cha Barcelona, Messi amewahi kuwa majeruhi kwa mwezi mmoja lakini timu hiyo iliendelea kushinda michezo yake bila wasiwasi.”

“Siwezi kukutajia majina mengine isipokuwa sina shaka la Kane ambaye ndiye mchezaji bora niliye naye.”

“Hata akianzia kwenye mechi au akitokea benchi lakini habari njema ni kwamba yupo tayari kurejea uwanjani kwa sasa kwani afya yake imeaimarika.”

“Hii ni habari njema kwetu na kwake. Ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chetu uwapo wake ni jambo la kufurahia.”

“Ni kuamua tu iwapo atatokea benchi au ataanza kwenye kikosi cha wachezaji 11, kikubwa ni kwamba amerejea uwanjani na ndiye straika tegemeo,” alisisitiza kocha huyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi