Wavuvi haramu 32 kutoka kayika kijiji cha Mgau wilayani Mtwara wanaojihusisha na uvuaji wa kasa wa baharini wamejisalimisha polisi kufuatia agizo la mkuu wa wilaya hiyo Evod Mmanda aliyewataka kujisalimisha wenyewe kabla ya kuanza kwa msako wa kuwakamata wavuvi haramu katika wilaya ya Mtwara.
Wavuvi hao ambao wameripoti polisi na kuachiwa kwa masharti ya kutorudia uvuvi huo na kutakiwa kuwa walinzi dhidi ya wavuvi wengine ambapo nyavu zao zipatazo sitini na nane zimeteketezwa moto na mkuu huyo wa wilaya.
Aidha Mmanda amesema kuwa operation ya kupambana na wavuvi haramu itaendelea kila kijiji kinachojihusisha na uvuvi.
Kwa upande wao wavuvi waliosalimu amri ya kuacha uvuvi wameiomba serikali kuwawesha kupata dhana halali za uvuvi ambazo wanadai zinauzwa bei kubwa madukani jambo ambalo linawafanya kutumia dhana haramu za uvuvi.