Mshambuliaji Depay avaa kama Michael Jackson

Paris, Ufaransa. Mshambuliaji Memphis Depay amepokea tuzo yake ya bao bora la mwaka akiwa amevalia jaketi mithili ya Michael Jackson.

Nyota huyo wa Uholanzi alinyakuwa tuzo hiyo baada ya kufunga bao la umbali akiwa nusu ya uwanja.

Depay (23), amekuwa katika mafanikio tangu alipondoka Manchester United na kujiunga na Lyon.

Muonekano wake katika tuzo za Mwanasoka bora wa Ufaransa uliwaduwaza wengi ukumbini hapo.

Nyota wa zamani wa Uholanzi, Frank de Boer aliwahi kumuonya Depay kwa kumtaka aweke akili yake zaidi uwanjani kabla ya kujiingiza katika mambo ya nje ya uwanja.

Baada ya kufunga mabao matano katika mechi15, ni wazi Depay sasa anahisi ni muda sahihi wa kurudi katika ulimwengu wake wa mitindo.
Mpya zaidi Nzee zaidi