Waethiopia wafariki wakati wakisafishwa kwenye kontena

WATU nane wanaodaiwa kuwa ni raia wa Ethiopia wamefariki dunia kwa kukosa hewa wakati wakisafirishwa kwa njia za panya katika kontena la gari kwenda nchini Afrika Kusini.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Dismas Kisusi, akizungumza na Nipashe Digital amesema tukio hilo limetokea jana saa 10.00 jioni katika kijiji cha Amani makolo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

Amesema Waethiopia hao ambao jumla walikuwa 33 walikuwa wakisafirishwa kwenye gari lenye mfumo wa kontena wakipelekwa Afrika kusini lakini walikosa hewa na kusabisha vifo hivyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi