Kibiti. Polisi mkoani Pwani imesema itawachukulia hatua kali za kisheria wananchi watakaobainika wanashirikiana na watu wanaofanya mauaji katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga.
Tukio la kuuawa kwa Katibu wa CCM wa Kata ya Bungu, Alife Mtulia aliyekuwa akiishi kijiji cha Nyambunda limefanya hadi sasa kufikisha idadi ya watu watano kuuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji hicho.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana iliyosainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga ilisema wahalifu wanaofanya mauaji hayo wanashirikiana na wenyeji kwenye maeneo husika.
Polisi pia imetoa wito kwa wananchi kuwafichua watu wote wanaowahisi wanashiriki katika matukio ya mauaji.
Kamanda Lyanga katika taarifa inayoelezea tukio la juzi la kuuawa kwa katibu huyo, pia amesema baadhi ya wenyeji wanawakumbatia wahalifu hao kwa kuwaficha.
Mauaji ya Mtulia ambaye pia alikuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma mbalimbali Februari 15, 2016 yamefanya idadi ya waliouawa kwa kupigwa risasi kufikia 30 katika wilaya hizo.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Mtulia aliuawa kwa kupigwa risasi nane sehemu mbalimbali mwilini na watu wawili ambao walimvizia alipokuwa anaenda kuoga nyumbani kwake.
Takwimu za matukio ya mauaji zinaonyesha kuwa watu wanne waliuawa Jumamosi kuamkia Jumapili na wawili waliuawa Jumapili kuamkia Jumatatu.
Mtulia, Mohammed Thabiti, Saidi Mbwana na Mohammed Malinda waliuawa Jumamosi kuamkia Jumapili kati ya saa 12:30 jioni na saa nne usiku.
Hemed Njiwa na Bakari Mpawane waliuawa Jumapili kuamkia Jumatatu kati ya saa 12:30 jioni na saa nne usiku.