Beki wa Yanga akiri kuzitamani posho za Stars

Beki aliyemaliza mkataba wake Yanga, Haji  Mwinyi amesema kuanguliwa kwa katika kikosi  cha Taifa Stars, kumenyima posho pamoja na  kujulikana kimataifa.

Mwinyi ni miongoni mwa wachezaji wa Zanzibar  waliondolea katika kikosi cha Stars kilichoenda

Misri kujiandaa na mechi ya kusaka kufuzu kwa  AFCON2019, dhidi ya Lesotho itakayocheza  Juni 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwinyi alisema hasara za kuenguliwa Stars ni kukosa posho zinazotolewa kwa wachezaji wanaokuwa kambini na timu hiyo.

"Tumeondolewa kutokana na Zanzibar kuwa  mwanachama wa CAF ni jambo zuri, kwani  imefika wakati wa Wazanzibari, kujitangaza  wenyewe hivyo viongozi wanatakiwa kuweka utaratibu mzuri wa kujua tutanufaika vipi," anasema

Mbali na posho, beki huyo anasema mchezaji  anayechezea timu ya taifa, anakuwa anajulikana na mataifa mbalimbali,hivyo inakuwa rahisi kupata dili nje.

"Jambo la kujivunia baadaye kwamba nilifanya kitu katika taifa kama wanavyotolewa mfano kina  Leodegar Tenga, wanaoonekana mfano kwenye taswira ya soka," anasema.
Mpya zaidi Nzee zaidi