Rais wa Zamani Ghana amvaa Trump

Rais wa zamani wa Ghana John Mahama amelaani uamuzi wa rais wa Marekakani , Donald Trump kwa kuiondoa Marekani kwenye makataba wa Paris wa 2015 kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

Bwana Mahama alituma ujumbe wake kwa njia ya Twitter, akiutaja uamuzi wa rais Trump wa kujiondoa kwenye makataba huo wa mazingira kama " jambo ambalo ni vigumu kuliamini". ''Ni siku ya huzuni sana katika ushirikiano wa kimataifa ". Uliandikwa ujumbe huo wa Bwana Mahama.

Rais huyo wa zamani wa Ghana alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa dunia waliunga mkono makubaliano hayo ya kihistoria juu ya mazingira mjini Paris, akiahidi kutekeleza hatua za kupunguza hewa ya makaa duniani.

AliTwitt wamba Marekani imejiondoa katika uongozi wake wa dunia.

Bwana Trump alisema kuwa mkataba huo "uliiadhibu" Marekani na utasababisha kupotea kwa mamilioni ya ajira nchini Marekani
Mpya zaidi Nzee zaidi