Queen Darleen alilipwa 500 na Dully Sykse Kisa?

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amefunguka kisa cha kuwahi kulipwa Tsh. 2,000 kwa ajili ya show katika maisha yake ya kimuziki.
Muimbaji huyo anayefanya vizuri kwa sasa na wimbo wake ‘Yono’, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa alikubali malipo hayo kutokana na kufanya muziki ili kupata umaarufu na warembo na si fedha.

“Niliamua kuwa msanii ili niwe maarufu nipate mademu tu na kupendwa na wasichana, wala sikufikiri kuwa msanii ili nipate pesa ndio maana hata nilipolipwa elfu mbili kwa ajili ya show nilikubali japo nilitakiwa kulipwa elfu tano, tena hiyo elfu mbili niliona nyingi na nikamlipa Queen Darleen mia tano sababu nilikwenda naye kwenye show,” amesema Dully Sykes.

Dully ameongeza kuwa hakuwahi kujua kama muziki ungekuwa biashara kama ilivyo sasa ambapo anafanya muziki kama biashara inayomlipa
Mpya zaidi Nzee zaidi