Waziri Mkuu Majaliwa Mgeni rasmi Fainali ya Mashindano ya Qu-ran Kidunia

Jumla ya Washiriki 18 kutoka mataifa mbalimbali Duniani wanatarajia kushiriki fainali ya  mashindano hayo yatakayo fanyika siku ya Ijumapili Juni 18, 2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

Kwamujibu wa Mjumbe wa kamati inayoratibu mashindano hayo Thabit Badi amesema mpaka sasa wameshawasili washiriki 15 na mpaka kufikia saa nane usiku kuamkia kesho watakuwa wamewasili wote.

Katika Fainali hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.
Mpya zaidi Nzee zaidi