TANESCO kumaliza tatizo la kukatikakatika umeme mkoani Lindi



 Anaripoti Ahmad Mmow Kutoka Lindi

TATIZO la kukosekana huduma za umeme za uhakika linaelekea kufika tamati kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme kilichojengwa katika kijiji cha Mahumbika. manispaa ya Lindi.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo hicho ambacho kitapokeaumeme kutoka Mtwara, Kaimu katibu mkuu wa wizara ya madini na nishati, Profesa James Mode, kwenye uzinduzi huo uliofanywa na waziri mkuu, Kasim Majaliwa.

Alisema kituo hicho ambacho ujenzi wake  umegharimu takribani shilingi 16 bilioni kitakuwa na kazi ya kupokea umeme toka Mtwara, kupoza na kusambaza katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu. Ikiwamo kwenye baadhi ya wilaya za mkoa huu. Ambazo ni Ruangwa, Nachingwea, Lindi na Liwale. Ambapo wilaya ya Kilwa inatumia umeme unaozalishwa Songosongo. Alisema serikali imejipanga kuwa na umeme wa uhakika na mwingi kwai kusambaza umeme wenye uwezo wa megawati 300.

Huku akibainisha kwamba matumizi ya juu ya umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni megawati 15. Ambapo sasa umeme unaozalishwa ni megawati 18. Hivyo umeme unaozalishwa ni mwingi. Hata hivyo serikali ipo kwenye mpango wa kuongeza megawati 4.

Kuhusu umeme vijiji, Profesa Mdoe alisema awamu ya tatu ya kusambaza umeme vijijini unaotekelezwa na wakala wa umeme vijijini (REA) utaanza kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Julai.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa usafirishaji na usambazaji umeme, mhandisi Kahitwa Bishaija alisema kituo hicho  ambacho  ujenzi wake umefamywa na kampuni tanzu ya TANESCO,inayotambulika kwa jina la Itideco, unalengo la kuboresha upatakanaji wa nishati hiyo. Nakubainisha kwamba ujenzi wa kituo hicho umefanyika kwa kipindi cha miezi minne tu.

 "Mitambo iliyopo hapa itafanyiwa majaribio tarehe 15 mwezi huu, licha ya kituo, TANESCO imejenga nyumba nne kwa ajili ya watumishi. Fedha zilizoyumika kwa ujenzi huu ni za ndani kwa asilimia 100," alibainisha Bishaija.

Bishaija alizitaja baadhi ya faida zilizopatikana kutokana na utekelezaji wa mradi huo kuwa ni kutoa ajira 430 kwa wananchi ambao wanaishi kwenye maeneo ambayo mradi huo umepita na kuimarika kwa uwezo wa wataalamu wa ndani. Kwa upande wake waziri mkuu, Kasim Majaliwa licha ya kuipongeza TANESCO, aliitaka kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote anae thubutu kukwamisha jitihada za serikali kusambaza umeme. Huku akiagiza kumwondoa mwananchi ambae alijenga nyumba kwenye njia iliyopitishwa umeme. Hata hivyo hataki kuondoka kwa hiari, ingawa alishalipwa finished. MWISHO.
Mpya zaidi Nzee zaidi