Yanga mbioni kuinasa saini ya Erasto Nyuni

Yanga wameanza kuiwinda saini ya Erasro Nyoni baada ya kocha wao, George Lwandamina raia wa Zambia kupendekeza asajiliwe kwa ajili ya kuziba pengo la kiungo mkabaji ambalo linaisumbua timu hiyo.

Jaffar Idd amesema kama Yanga wana nia ya kweli ya kumtaka Nyoni basi wawafuate mezani kwa ajili ya kujadiliana nao juu ya bei ya kuwauzia.

“Tunasikia tu kwamba nyota wetu fulani wanatakiwa na Yanga lakini wenyewe bado hawajatufuata kwa ajili ya kuzungumza nasi kujadili bei za kuwauzia nyota hao ambao wanawataka,” alisema Idd.
Mpya zaidi Nzee zaidi