Musoma: Wananchi wamkataa mwenyekiti wao kwa madai ya kuongoza kibaguzi.

Wananchi wa mtaa ya Nyabisarye katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamemkataa Mwenyekiti wao wa serikali ya mtaa huo kwa madai ya kuongoza wananchi kwa misingi ya ubaguzi wa kisiasa na kikabila huku akishindwa kusomea wananchi taarifa za mapato na matumizi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara mbele ya mkuu wa wilaya ya Musoma Dk Vicent Naano,wananchi hao wameitaka serikali kuchukua hatua za kutatua mgogoro huo, ambao wamedai umesababisha sasa washindwe kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika mtaa huo.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa serikali ya mtaa wa Nyabisarye Bw Samwel Gabayala,akizungumza katika mkutano huo wa hadhara ambao umeitishwa kwa lengo la kutatua mgogoro huo,amekanusha kuongoza mtaa huo kwa misingi ya ubaguzi,huku akisema kuwa wananchi wake wamekuwa kikwazo kwa kukishindwa kufika katika mikutano ya hadhara ambayo imekuwa ikitishwa kwa ajili ya kusomwa mapato na matumizi.

Naye mkuu wa wilaya ya Musoma Dk Vicent Naano,akizungumza katika mkutano huo,amewaonya viongozi wa mtaa wanaoshindwa kuhamasisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao badala yake kuongoza wananchi kwa misingi ya ubaguzi wa kisiasa.
Mpya zaidi Nzee zaidi