Profesa Lipumba akwama mahakamani

Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake wamekwama mahakamani leo baada ya Jaji Ndyansobera kukataa maombi ya Profesa Lipumba na kundi lake.

Jaji Ndyansobera amekataa kufuta kesi Namba 28/2017 kama ilivyoombwa na Lipumba ili wapate Ruzuku ya Chama  Cha Wananchi wa CUF inayofikia shilingi billion moja na million mia nne toka Julai mwaka jana.

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Mbarala Maharagande amefunguka na kusema kufuatia maamuzi haya ya mahakama hivyo hakuna pesa ambayo Profesa Lipumba anaweza kuchukua hata shilingi moja.